Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 11:51

Niger yasitisha kwa muda idhini ya kusafirisha mafuta Mali


Eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

Niger imesitisha kwa muda kutoa idhini ya kusafirisha bidhaa za mafuta hadi nchi jirani ya Mali isipokuwa kama zinapelekwa kwa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Katika taarifa ya serikali Septemba 21 ambayo Reuters imeweza kupata leo Jumanne, Niger ilisema pia inafutilia mbali idhini ambayo tayari imetolewa, lakini haikutaja sababu za hatua hiyo.

Niger ni mojawapo ya nchi chache za Afrika Magharibi ambazo husafisha mafuta ya kutosha kwa ajili ya soko la ndani kutoka kwenye kiwanda kidogo cha kusafisha mafuta chenye uwezo wa kufikia mapipa 20,000 kwa siku . Uzalishaji wa ziada unasafirishwa kwenda nchi zingine katika kanda ya Afrika Magharibi.

Umoja wa Mataifa una ofisi ya kulinda amani nchini Mali ili kusaidia kupambana na waasi wa Kiislamu.

Msemaji wa serikali ya Mali hajapatikana ili kutoa maoni yake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG