Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 04:17

Niger yapoteza wanajeshi wake katika mapambano na Boko Haram


Niger's special forces prepare to fight Boko Haram in Diffa, March 26, 2015. Niger said it lost 46 soldiers and 28 civilians in weekend clashes with the Islamist militants.
Niger's special forces prepare to fight Boko Haram in Diffa, March 26, 2015. Niger said it lost 46 soldiers and 28 civilians in weekend clashes with the Islamist militants.

Serikali ya Niger inasema wanajeshi 46 na raia 28 waliuwawa mwishoni mwa juma wakati vikosi vikipambana na wanamgambo wa Boko Haram kudhibiti kisiwa kimoja katika ziwa Chad.

Maafisa wanasema kwamba wanamgambo156 pia waliuwawa katika mapambano ambayo yalianza baada ya Boko Haram, kushambulia kisiwa cha Karamga siku ya Jumamosi.

Jeshi la Niger linasema toka kipindi hicho wamefanikiwa kushikilia kisiwa hicho.

Niger, pamoja na Nigeria, Chad na Cameroon, siku za karibuni zimemekuwa zikifanya mashambulizi kumaliza kadhia inayofanywa na Boko Haram.

Mpaka sasa Boko Haram, imesha gharimu maisha ya watu 10,000 na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni moja kaskazini mashariki mwa Nigeria.

XS
SM
MD
LG