Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 08:06

Niger, Mali na Burkina Faso zajiondoa kwenye Jumuia ya ECOWAS


Nembo ya ECOWAS
Nembo ya ECOWAS

Nchi tatu za Afrika Magharibi zinazoongozwa na wanajeshi, Niger, Mali na Burkina Faso Jumapili zimesema zinajiondoa kwenye Jumuia ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ( ECOWAS), kulingana na taarifa ya pamoja iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa ya Niger.

“Baada ya miaka 49, watu mashujaa wa Burkina Faso, Mali na Niger kwa masikitiko makubwa wanaona kwamba ECOWAS haizingatii tena maadili ya waasisi wake na msingi wa Afrika iliyoungana,” msemaji wa utawala wa kijeshi wa Niger, Kanali Abdramane Amadou amesema katika taarifa.

Ameongeza kuwa “ Jumuia hiyo ilishindwa kabisa kuzisaidia nchi hizo katika vita vyao dhidi ya ugaidi na usalama mdogo.”

Forum

XS
SM
MD
LG