Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:44

Trump aelezea sera zake za mambo ya nje


Donald Trump
Donald Trump

Donald Trump, ambaye anaongoza katika uchaguzi wa awali wa kuwania tikiti ya chama cha Republican, jana Jumatano alieleza nia yake ya kufanya mabadiliko makubwa katika sera za mambo ya nje, huku akisema kwamba angependa Marekani ije kwanza. Aliongeza kuwa Marekani kwa sasa iko katika hali mbaya.

Trump, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mwendeshaji wa makala ya televisheni yaliyomulika maisha ya kila siku, na ambaye hajawahi kushikilia afisi ya umma, hakuwa ameeleza kinaga ubaga malengo yake kuhusu sera za mambo ya nje. Lakini kwenye hotuba ya dakika 38 katika hoteli moja hapa Washington, DC, Trump alimshambulia Rais wa sasa Barack Obama na kusema haridhishwi na jinsi rais huyo anavyotekeleza wajibu wake katika maswala ya kigeni.

Aidha, Trump alimkosoa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Hillary Clinton. Bi Clinton huenda akawa mgomea wa urais wa chama cha Demokratik na huenda wawili hao wakakabiliana katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba mwaka huu.

XS
SM
MD
LG