Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:13

Ni uhalifu kumuambukiza mtu HIV kwa maksudi Uganda


Uganda parliament in session
Uganda parliament in session
Mswada huu ukiwa sheria utawaadhibu watu walio na virusi vya HIV ambao watawaambukiza wenzao kwa makusudi. Uganda, imekuwa kwenye msitari wa mbele tangu miaka ya tisini kwenye vita dhidi ya ukimwi.

Mswada huu uliowasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka wa 2010, una kipengele kimoja ambacho kimekuwa na utata mkubwa.

Kipengele hiki kinasema ikiwa mtu anajua anaugua ugonjwa wa ukimwi, atakuwa na jukumu la kumwambia mpenzi wake kwamba ana virusi vya ukimwi kabla ya kushiriki ngono, na pia atakuwa na jukumu la kufuata maagizo ya maafisa wa afya ya jinsi ya kushiriki ngono ili asimwambukize mwenzake. Ikiwa hatofanya hivyo na akamwambukize mwenzake virusi vya HIV, basi hilo litakuwa kosa na ataadhibiwa kifungo cha maisha gerezani.

Kasisi Gedion Byamugisha ni mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu na anaishi na virusi vya ukimwi anaema, "Nadhani kuna sababu tatu zinazonifanya ni hisi kwamba kipengelechenye utata cha 41 chafaa kufutiliwa mbali. Kwanza, kinamwangalia tu mtu mmoja ambaye ni mtu anayeishi na ukimwi."

Kasisi Byamugisha anaendelea kueleza kamba "Mbona hakina adhabu zitakazotolewa kwa watu wengine ambao wataambukizwa ukimwi? Mbona umwadhibu anayeambukizana na umwache anayeambukizwa ambaye huenda alishiriki ngono bila kinga au hakumwambia mpenzi wake waende wapimwe kabla ya kushiriki ngono? Kama ni kesi za ubakaji basi wanaoambukizana waadhibiwe lakini kama watu wawili walio komaa wanakubaliana, basi hilo halifai."

Anayeambukizwa ana jukumu la kujikinga. Sauti zingine zinazopinga mswada huu kama zile za wanasheria zinauliza utathibitisha namna gani kwamba fulani alikuwa na lengo la kumwambukiza mwenzake virusi vya ukimwi.

Pili, mtu akidai kwamba mshtakiwa ana virusi vya ukimwi, atawezaje kuthibitisha kwamba wakati akishiriki ngono naye tayari alikuwa na hivyo virusi?

Kwa mujibu wa takwimu za tume ya ukimwi nchini Uganda, kiwango cha maambukizi kimepanda na kufikia asili mia saba nukta tatu. Miaka mitatu iliyopita kilikuwa asili mia sita.

Maafisa wa afya nao wanasema Uganda miaka ya tisini ilipiga hatua dhidi ya ukimwi kwa sababu uliwahamasisha watu kuhusu umuhimu wa kupimwa ili kujua kama wana ukimwi. Huu mswada ambao utakuwa sheria ikiwa rais atautia saini, umekosolewa na watu wengi wakisema utawafanya watu kuhofia kwenda kupimwa.
XS
SM
MD
LG