Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 12, 2025 Local time: 01:59

Nguvu za mahakama 'kupunguzwa' Israel, waandamanaji wamejitokeza


Mamia ya waandamanaji wakiandamana kuelekea Jerusalem, kupinga mswada wa kufanyia marekebisho mfumo waa mahakama. July 22, 2023.
Mamia ya waandamanaji wakiandamana kuelekea Jerusalem, kupinga mswada wa kufanyia marekebisho mfumo waa mahakama. July 22, 2023.

Bunge la Israel linapiga kura hii leo kuhusu mswaada wa kubadilisha utendakazi wa mahakama ambo unaungwa mkono na waziri mkuu Benjamin Netanyahu, ambao umepelekea maandamano katika muda wa miezi kadhaa.

Melfu ya waandamanaji wamejitokeza barabarani mjini Jerusalem kupinga mapendekezo ya Netanyahu kupunguza nguvu za majaji, hatua ambayo wakosoaji wake wanasema utadunisha mfumo wa demokrasia wa Israel.

Wabunge waliujadili mswaada huo jumapili, hadi usiku.

Polisi wametumia maji kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliofunga lango kuu la kuingia bungeni, leo Jumatatu.

Netanyahu anatarajiwa bungeni wakati wa upigaji kura kuhusu mswaada huo, licha ya kwamba ametoka hospitali siku chache zilizopita ambako aliwekewa kifaa cha kusaidia moyo wake kufanya kazi.

Miongoni mwa maswala yenye utata kwenye mswaada huo ni kupunguza uwezo wa mahakama kuu kubadilisha maamuzi ya bunge, pamoja na kubadilisha mchakato wa kuteua majaji.

Forum

XS
SM
MD
LG