Waziri mkuu wa New Zealand Chris Hipkins amesema kwamba kanuni za kuvaa barakoa kwenye hospitali pamoja na maeneo mengine ya afya zitaondolewa usiku wa manane, zikiwemo zile pia zilizohitaji mtu aliyeambukizwa kujiweka karantini kwa siku 7. Mwanzoni New Zealand ilisifiwa kimataifa kutokana na kuangamiza kabisa kirusi hicho, kufuatia kufungwa kwa shughuli za kawaida kote nchini pamoja na kuweka sheria kali za usafiri kwenye mipaka. Hata hivyo kadri janga lilivyoendelea kuenea, pamoja na kujitokeza kwa aina tofauti za virusi , taifa hilo lililegeza baadhi ya juhudi zake baada ya kugundua kuwa hazikuwa zikifanya kazi.
Forum