Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:06
VOA Direct Packages

New Zealand yaendelea kukadiria hasara baada ya kimbunga Gabrielle


Picha ya mafuriko yaliosababishwa na kimbunga Gabrielle karibu na mji wa Napier. AFP February 14 , 2023
Picha ya mafuriko yaliosababishwa na kimbunga Gabrielle karibu na mji wa Napier. AFP February 14 , 2023

New Zealand imeanza mchakato wa ukaguzi na ukadiriaji wa hasara iliyosababishwa na kimbunga Gabrielle ambacho kimeondoka nchini Jumatano.

Takriban watu wanne wamethibitishwa kufa kutokana na kimbunga hicho kinachosemekana kuwa kibaya zaidi kuwahi kupiga taifa hilo la Pacific, akiwemo zima moto mmoja wa kujitolea ambaye alifunikwa na maporomoko ya ardhi kwenye ufukwe wa mashariki mwa taifa.

Mwingine alikuwa mtoto mdogo aliyesombwa na maji Jumanne kwenye makazi ya Eskdale karibu na ufukwe wa Hawke Bay ulioko kwenye kisiwa cha North Island. Kimbunga hicho kilichopiga taifa hilo Jumatatu kilikuwa na mvua za hadi centimita 40, zilizopelekea mafuriko, maporomoko ya ardhi pamoja na uharibifu wa miundombimu muhimu.

Takriban wakazi 9,000 wamelazimika kuondoka kwenye nyumba zao huku wengine wakilazimika kuchukua hifadhi kwenye mapaa ya nyumba zao ili kujiepusha na mafuriko. Serikali imesema kwamba zaidi ya watu 1,400 kutoka North Island hawajulikani walipo wakati nyumba zilizokosa umeme zikishuka kutoka 225,000 hadi takriban 144,000 kufikia leo.

XS
SM
MD
LG