Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:37

New York yaanza kanuni mpya za Covid-19


Watu wakitembea mjini New York
Watu wakitembea mjini New York

NewYorkJumanne imeanza kutumia kanuni mpya inayohitaji kila mmoja mwenye umri wa miaka 12 kuendelea, aonyeshe ushahidi kwamba amepokea chanjo ya covid kabla ya kuruhusiwa kuingia kwenye maeneo ya umma kama vile migahawa, vyumba vya burudani au kwenye biashara nyingine. 

Kulingana na mtandao wa serikali ya jimbo la New York, ushahidi unaokubalika ni pamoja na kadi iliyotolewa na idara ya kudhibiti magonjwa ya Marekani, CDC, kibali maalum kinachotolewa na mamlaka ya jiji au kupitia App maalum kwenye simu ya mkononi kwa jina NYC Covid Safe. Picha ya kadi iliyotolewa na CDC, pia inakubalika.


Maafisa wa jiji wanasema kuwa ingawa kanuni hiyo ilianza kutumika Jumanne, hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi ya wanaoikiuka hapo Septemba 13. Biashara ambazo zitapatikana kukiuka kanuni hizo pia zitatozwa faini. Meya wa New York Bill de Blassio ameambia wanahabari Jumanne kwamba wafanyabiashara wengi wamekaribisha hatua hiyo kwa kuwa wanataka usalama kwa wafanyakazi wao.

XS
SM
MD
LG