Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:37

Ghasia zazuka Bujumbura wakati wa ziara ya Wajumbe.


Ghasia za awali mjini Bujumbura.
Ghasia za awali mjini Bujumbura.

Ghasia zimeshudiwa usiku wa kuamkia Ijumaa katika kata mbali mbali za mji ya Bujumbura, Burundi, ambapo milio ya risasi na milipuko mingine imesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine kumi na watatu.

Msemaji wa polisi ameandika kwenye mtandao wake wa tweeter kuwa miongoni mwa waliouwawa ni wahalifu wawili na raia wa kawaida mmoja. Haya yamejiri wakati wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa walipokuwa wakikamilisha ziara yao ya siku mbili nchini humo, ambapo Ijumaa jioni walipokelewa na Rais Pierre Nkurunziza kwa mazungumzo katika mkoa ulio kati kati mwa Burundi wa Gitega.

Awali, wajumbe hao walikutana kwa mazungumzo na makamu wa kwanza wa rais Gaston Sindimwo. Mara walipowasili Alhamisi usiku, wajumbe hao walipata nafasi ya kukutana na marais wawili wa zamani wa Burundi.

XS
SM
MD
LG