Wizara ya mambo ya Nje ya Iran imeviita vikwazo vipya vilviyowekwa na Marekani vinavyolenga mpango wake wa makombora kuwa si halali. Msemaji wa wizara hiyo HOSSEIN JABER ANSARI amesema leo kwamba Iran itajibu kwa kuboresha juhudi zake kwa program halali ya makombora na kuhamasisha uwezo wake wa kujilinda.
Iran ilishutumiwa na Marekani na mataifa mengine ya magharibi kwa kufanya majaribio ya makombora mara mbili mwishoni mwa mwaka jana, huku wakisema hatua hiyo ilikiuka maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa. Lakini iran ilitetea majaribio hayo kuwa ni suala la usalama wa kitaifa.