Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:37

Ndoa za utotoni zaongezeka barani Afrika


Msichana mmoja kutoka Nigeria
Msichana mmoja kutoka Nigeria

Ingawa ni kinyume cha sheria kuoza wasichana walio chini ya umri katika nchi nyingi za Afrika, lakini waatalamu wanasema utekelezaji wa sheria hizo hauna nguvu na mila ya kale kuelekea wasichana na wanawage ingali na nguvu.

Takwimu mpya zinaonyesha viwango vya kushtusha vya kuongezeka kwa ndoa za utotoni barani Afrika, na kusababisha waatalamu kukutana pamoja nchini Zambia kujadili namna ya kukomesha mila hiyi.

Ingawa ni kinyume cha sheria kuoza wasichana walio chini ya umri katika nchi nyingi za Afrika, lakini waatalamu wanasema utekelezaji wa sheria hizo hauna nguvu na mila ya kale kuelekea wasichana na wanawage ingali na nguvu.

Idadi ya watu barani Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa mara mbili miaka 35 ijayo, na iwapo mwenendo wa sasa hautabadilika, basi hata idadi ya wasichana watakaoozwa itaongezeka vivyo hivyo, na kufikia milioni 310.

Ripoti mpya iliyotayarishwa na Idara ya umoja wa mataifa kwa ajili ya watoto, UNICEF inaeleza kwamba endapo mambo hayatabadilika, ifikapo mwaka 2050, basi karibu nusu ya watoto wanaoolewa mapema duniani watakuwa barani Afrika.

Huko nchini Zambia wiki hii, umoja wa Afrika unaendelea na mkutano wa viongozi kuhusu jinsi ya kumaliza ndoa za watoto. Kongamano hilo linatarajiwa kupitisha azimio kwamba umri wa miaka 18 uwe kigezo cha msichana kuolewa barani kote.

Ndoa kabla ya miaka 18 imepigwa marufuku katika nchi nyingi za Afrika hata hivyo kama Marekani baadhi ya nchi zinaruhusu viijana kuoa kwa ridhaa ya wazazi wao.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma anasema tamaduni zinazowadhalilisha wasichana na wanawake ndio wa kulaumiwa. Wataalam wanasema kwamba umaskini na ukosefu wa nafasi za masomo pia zinachangia hali hiyo.

Kaimu Mkurugenzi kitengo cha UNICEF cha usalama wa mtoto, Cornelius Williams, anasema utafiti unaonyesha kwamba ndoa za utotoni zina athari nyingi, na baadhi yake huenda zikaleta hata mauti.

XS
SM
MD
LG