Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 07:19

Ndege ya mizigo yaanguka Sudan Kusini


Muonekano wa ndege aina ya Antonov 12 ikiwa safarini
Muonekano wa ndege aina ya Antonov 12 ikiwa safarini

Ndege moja imeanguka nchini Sudan Kusini muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi wa Juba na kuuwa watu wasiopungua 25.

Ripoti zilieleza ndege ya mizigo aina ya Antonov ilianguka mita 800 kutoka kwenye njia ya kuondokea ndege hapo Jumatano na kutua kwenye eneo la msitu mnene kwenye ufukwe wa mto Nile.

Taarifa za awali kutoka kwa walioshuhudia, waandishi wa habari na ofisa wa serikali zilisema inaaminika watu wasiopungua 25 wamefariki huku kukiwa na watoto kadhaa.

Ndege ya mizigo iliyopata ajali Juba, Nov. 4, 2015.
Ndege ya mizigo iliyopata ajali Juba, Nov. 4, 2015.

Radio shirika ya Umoja wa Mataifa iitwayo Miraya iliwakariri mashahidi wakisema wamehasabu miili ipatayo 40 iliyoonekana kwenye mabaki hayo.

Ripoti za habari zilisema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikielekea kwenye vinu vya mafuta vya Paloch katika jimbo la Upper Nile State. Ripoti kutoka eneo yalipo mabaki ya ndege hiyo zinasema ndege hiyo ilionekana kubeba shehena ya chakula pamoja na abiria.

Haijafahamika mara moja kama waathirika wote walikuwa ndani ya ndege au iwapo baadhi ya waathirika walikuwa kwenye eneo wakati ajali ilipotokea.

XS
SM
MD
LG