Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:54

Ndege ya Mike Pence yateleza na kutoka kwenye njia yake New York


Ndege ya kampeni ya Mike Pence.
Ndege ya kampeni ya Mike Pence.

Ndege iliyokuwa inamsafirisha mgombea mwenza wa urais wa chama cha Republikan Mike Pence iliteleza kutoka njia yake wakati wa mvua kubwa ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa LaGuardia New York.

Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo na Mike Pence alionekana kwenye Televisheni akisimama nje ya ndege hiyo na kuwapa mkono wafanyakazi wa zima moto waliokimbilia kwenye eneo la ajali.

Njia ya ndege ilikuwa na maji mengi na kuteleza kutokana na mvua zilizonyesha na baridi. Abiria walieleza kwamba ndege ilitua kwa mtikisiko mkubwa na kusema kulikua na harufu ya mipira ya matairi ikiungua pale rubani alipokua anaweka breki kali.

Mwandishi wa CNN aliyekuwa kwenye ndege hiyo anasema yeye na karibu abiria 30 hadi 40 wengine wako salama lakini wamestushwa sana.

XS
SM
MD
LG