Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:23

Ndege ya kwanza inayotumia nguvu za jua yajaribu kuvuka milima ya Morocco.


Ndege inayotumia mionzi ya jua.
Ndege inayotumia mionzi ya jua.

Mafisa wa Solar Impulse wametangaza Jumatano kwamba upepo mkali na misuko suko hewani kati ya Cassablanca na Marakesh imesababisha ndege hiyo kuahirisha safari.

Habari hizo zilizotangazwa kwenye tovuti ya Solar Impulse inasema rubani hakuwa hatarini lakini mkurugenzi wa safari aliamuamrisha kurudi kutokana na hofu juu ya hali ya hewa ambayo ilikuwa haitabiriki.

Ndege hii ya kwanza inayotumia nguvu za jua iliyofanya safari yake ya kwanza kati ya Hispania na Morrocco wiki iliyopita, iliruka kutoka mji mkuu Rabat Jumatano saa mbili asubuhi ikiendeshwa na rubani mfanyabiashara Mswissi Andre Borchberg ilijaribu kusafiri kusini kuelekea mji wa Ouarzazate.

Safari hiyo ilikuwa ni sehemu ya mpango wa Morocco kuzindua kiwanda cha kwanza kikubwa cha nguvu za jua katika eneo hilo la jangwa ifikapo mwaka 2014.

Timu ya Solar impulse ya Switzerland imekuwa ikifanya kazi na serikali ya Morocco kuhamisha matumizi ya teknolojia mbadala ya nishati.

Rubani huyo wa Kiswissi amesema safari hiyo ya jangwani ni nafasi nzuri pia kwa shirika lake la Solar Impulse kujifunza kabla ya kufanya ziara ya kuzunguka dunia nzima 2014.

XS
SM
MD
LG