Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:31

Kenya kuwasilisha malalamiko dhidi ya ICC


Amina Mohamed, Kenya
Amina Mohamed, Kenya

Mkutano wa 14 wa nchi zilizounda mahakama ya ICC ulifunguliwa mjini Hague, Uholanzi, jana Alhamisi. Mataifa mengi yanawakilishwa kwenye mkutano huo ambao unaendelea kujadili maswala yanyohusu mahakama hiyo, ambayo iliundwa mwaka wa 2002 kwa madhumuni ya kuyasaidia mataifa wanachama kusikiliza na kutatua kesi za jinai, na mauaji ya kikabila au kimbari.

Na BMJ Muriithi

Mkutano wa 14 wa nchi zilizounda mahakama ya ICC ulifunguliwa mjini The Hague, Uholanzi, siku ya Alhamisi. Mataifa mengi yanawakilishwa kwenye mkutano huo ambao unaendelea kujadili maswala yanyohusu mahakama hiyo, ambayo iliundwa mwaka wa 2002 kwa madhumuni ya kuyasaidia mataifa wanachama kusikiliza na kutatua kesi za jinai, na mauaji ya kikabila au kimbari.

Katika mkutano huo Kenya ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotarajiwa kuwasilisha hoja yake Ijumaa kuhusu swala la kipengele cha 68 cha sheria za mahakama hiyo, ambacho kimezua utata baada ya amri kwamba ushahidi uliobatilishwa au kukanwa, utumike kwenye kesi zinazowakabili naibu wa rais wa Kenya, Willaim Samoei Arap Ruto na mwanahabari Joshua Sang kwenye mahakama hiyo.

Kulikuwa na vuta nikuvute kati ya ujumbe wa Kenya ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo, Amina Mohamed na upande wa Mashtaka ukiongozwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda.

Bi Muhamed alisema kuna umuhimu wa hoja iliyowasilishwa na Kenya kusikilizwa na kuongeza kwamba huu ni wakati mwafaka wa kuhakikisha kwamba kuna usimamizi huru wa shughuli za mahakama hiyo ya ICC.

Lakini Kiongozi wa mashtaka alipinga vikali huku akisema kwamba maswala ya mahakama hayafai kuzungumziwa nje ya koti

Umoja wa Afrika unaiunga mkono serikali ya Kenya na unahoji hatua ya mahakama hiyo kutumia ushahidi huo ambao ulibatilishwa au kukanwa.

Kenya imetuma ujumbe mkubwa kuiwakilisha kwenye kikao hicho huku wabunge wengi wanaomuunga mkono naibu wa Rais Ruto wakiandamana na ujumbe huo wa serikali.

Mbali na kesi ya Wakenya hao, nchi wanachama zitawasilisha hoja ambazo zingependa kujadiliwa hili kuimarisha mstakabal wa mahakama hiyo ya ICC.

XS
SM
MD
LG