Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:31

Nato yasikitishwa na kupotea kwa maisha ya raia


Nato yasikitishwa na kupotea kwa maisha ya raia

Nato yaeleza tatizo la mfumo wa silaha lasababisha kombora kupoteza shabaha.

NATO inasema shambulio la kimakosa na majeshi yake linaweza kuwa limeuwa raia katika mji mkuu wa Libya Tripoli .

Muungano huo umesema jumapili kuwa mashambulizi hayo ya anga yalilenga eneo la kijeshi la makombora lakini silaha moja haikulenga shabaha yake kutokana na uwezekano wa mfumo wa silaha hiyo kutokufanya kazi sawa sawa .

NATO imesema inasikitishwa na kupotea kwa maisha ya raia.

Maafisa wa Libya wanasema shambulizi la anga la NATO lilipiga kwenye eneo la mtaa wanaoishi raia na kuuwa watu 9 ikiwa ni pamoja na watoto 2.

XS
SM
MD
LG