Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 23:34

Mashambulizi ya anga ya NATO yashutumiwa kumjeruhi Gadhafi


Jengo mojawapo lililoharibiwa na oparesheni ya anga ya NATO kwenye eneo la kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi
Jengo mojawapo lililoharibiwa na oparesheni ya anga ya NATO kwenye eneo la kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi

Waziri wa mambo ya nje wa Italy, Franco Frattini anasema kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi amejeruhiwa baada ya wiki kadhaa za mashambulizi ya anga ya NATO nchini Libya.

Frattini aliwaambia waandishi wa habari leo Ijumaa kwamba alipata habari kutoka kwa askofu mmoja wa kikatoliki mjini Tripoli, Giovanni Martinelli, kwamba bwana Gadhafi huenda amejeruhiwa na ameondoka mjini humo.

Msemaji wa serikali ya Libya amekanusha ripoti hiyo na kuiita ni upuuzi mtupu. Tripoli imekuwa ni eneo la mashambulizi mazito ya NATO, baadhi yakipiga karibu na maeneo ya bwana Gadhafi. Kiongozi wa Libya pia ameripotiwa kuepuka shambulizi moja la karibuni ambalo maafisa wa Libya wanasema lilimlenga yeye. NATO imekanusha kumlenga kiongozi wa Libya.
Hapa Washington leo Ijumaa, Rais wa Marekani Barack Obama anakutana na katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, kuzungumzia operesheni ya ushirika inayoendelea nchini Libya.

Tofauti na hayo, ujumbe wa Baraza la taifa la mpito -TNC nchini Libya, wamekutana na mshauri wa usalama wa taifa wa bwana Obama, Tom Donilon, siku moja baada ya kupata uungaji mkono mkubwa wa kisiasa kutoka Uingereza.

Waziri wa fedha na mafuta wa TNC, Ali Tarhouni aliiambia Sauti ya Amerika baada ya mkutano kwamba uongozi wa upinzani unashukuru msaada wa Marekani, lakini wanataka kutambuliwa kisiasa na kuwa na fursa ya kupata mali serikali ya Gadhafi ambazo zimezuiliwa.

Kundi hilo pia linataka silaha za kisasa na mahitaji ya msingi kama vile chakula, madawa na mafuta.

XS
SM
MD
LG