Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:44

National Alliance yakaribisha utiaji saini wa Sudan Kusini


Timu ya wapatanishi wa mgogoro wa Sudan Kusini katika mazungumzo mjini Addis Ababa
Timu ya wapatanishi wa mgogoro wa Sudan Kusini katika mazungumzo mjini Addis Ababa

Ushirika wa vyama vya siasa vya upinzani nchini Sudan Kusini wa National Alliance vilikaribisha utiaji saini wa mkataba wa maridhiano uliofikiwa kati ya wafungwa wa zamani wa kisiasa na upinzani wa SPLM. Katika taarifa ushirika huo pia uliitaka serikali kutia saini makubaliano hayo.

Kiongozi wa kundi, Dr.Lam Akol alisema masuala mengi yaliyopendekezwa katika mkataba yalishajadiliwa na watu kwa takribani mwezi mmoja. Alisema kile kinachohitajika hivi sasa ni kwa viongozi kufanya maamuzi magumu.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na mpinzani wake, Riek Machar.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na mpinzani wake, Riek Machar.

Serikali haikutia saini mkataba wa Agosti 17, ikisema inahitaji muda zaidi wa kushauriana. Hata hivyo serikali inatarajiwa kutia saini mkataba hapo Septemba mosi.

XS
SM
MD
LG