Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:55

Naibu katibu mkuu wa UM azungumza na Taliban


Mwanadiplomasia wa juu  wa Umoja wa Mataifa alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan.

Mazungumzo hayo ni kwa ajili ya kuwasilisha wasiwasi wa kimataifa kuhusu marufuku iliyowekwa kwa wanawake ya kufanyakazi, elimu na maisha kiujumla.

Naibu Katibu Mkuu, Amina Mohammed, mwanamke wa ngazi ya juu zaidi katika taasisi hiyo ya dunia, aliwasili katika mji mkuu, Kabul, akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa.

Ziara yake ameifanya karibu mwezi mmoja toka Wanamgambo wenye msimamo mkali wa Taliban kuongeza masharti yao dhidi ya wanawake wa Afghanistan.

Marufuku hizo ziliwaamuru wafanyakazi wengi wa mashirika ya kiraia wa kike kuacha kazi hadi pamoja na marufuku nyingine ya kuwazuia wasichana kuhudhuria vyuo vikuu.

XS
SM
MD
LG