Watu waliokoseshwa makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Minawao iliyoko kwenye mpaka wa kaskazini mwa Cameroon karibu na Nigeria, wanasema kwamba idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu inaendelea kuongezeka kila siku.
Toudje Voumou ambaye ni afisa wa ngazi ya juu wa serikali kwenye wilaya ya Mayo Moskota, amesema kwamba kikosi kazi cha pamoja cha tume ya ziwa Chad, MNJTF, kimeimarisha uwepo wake kwenye mpaka huo. Kikosi hicho kina wanajeshi kutoka Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.
Serikali ya Cameroon imesema kwamba wanavijiji wanahitaji kushirikiana na vikosi vinavyopigana na wanajihadi kwa kutoa ripoti ya watu wageni miongoni mwao. Serikali imesema kwamba imeanza kutumia vikosi vya ziada ili kusaidia kwenye vita hivyo.
Wakati wa ziara yake ya Aprili 2022 nchini Cameroon, mkuu wa shirika la wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa Filippo Grandi, aliahidi kutoa msaada zaidi kwa watu waliokoseshwa makazi pamoja na wakimbizi wanaokimbia mapigano na majanga ya kiasili.
Hata hivyo UN inasema kwamba imepokea asilimia 23 pekee ya dola milioni 100 zinazohitajika, ili kuwasaidia wakimbizi kwenye taifa hilo la Afrika ya kati.
Facebook Forum