Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 21:26

Mzozo wa Thailand waongezeka


Waandamanaji wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra mjini Bangkok May10, 2014
Waandamanaji wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra mjini Bangkok May10, 2014

Afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi anasema jaribio la kumteuwa waziri mkuu ambaye hakuchaguliwa huenda likatumbukiza nchi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Thailand inasema inaimarisha ulinzi kabla ya maandamano ya kesho Jumatatu kati ya makundi yanayounga mkono serikali na yale yanayoipinga.

Hatua hiyo inafuatia kujeruhiwa kwa watu wawili karibu na makao makuu ya serikali Jumamosi jioni katika mlipuko wa gruneti.

Katika tangazo kupitia televisheni ya kitaifa, maafisa wa serikali ya muda walionya watu wakae mbali na maeneo ya maandamano hayo kwa usalama wao.

Waandamanaji wanaopinga serikali hiyo wametoa mwito kuteuliwe Waziri Mkuu anayekubalika na pande zote kesho Jumatatu.

Afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi Tharit Pengdit anasema jaribio la kumteuwa Waziri Mkuu ambaye hakuchaguliwa huenda likatumbukiza Thailand katika ghasia zaidi na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.
XS
SM
MD
LG