Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:55
VOA Direct Packages

Mzozo wa kisiasa watokota Sudan Kusini kati ya rais na makamu wake


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, mwenye kofia, na makamu wake wa rais Riek Machar.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, mwenye kofia, na makamu wake wa rais Riek Machar.

Mabadiliko ya kushtukiza yaliyofanywa mwezi huu kwenye baraza la mawaziri na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir yamezua wasiwasi kuhusu uthabiti wa kisiasa nchini humo.

Upinzani kwenye serikali ya mpito ya Juba umeomba rais kubatilisha hatua hiyo au ahatarishe amani ya taifa hilo. Makamu wa Rais Riek Machar amesema kwamba iwapo Kiir hatafuata ushauri huo, basi huenda akalazimika kuchukua hatua mbadala.

Baada ya rais Salva Kiir kutangaza mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri zaidi ya wiki moja iliyopita, wakazi wengi wa Sudan walichukulia hatua hiyo kama mojawapo tu, ya amri zake ambazo kwa kawaida husomwa kupitia televisheni ya kitaifa.

Lakini kwa Riek Machar ambaye ni hasimu wa kisiasa wa Kiir, na pia makamu wake wa rais, kufukuzwa kazi kwa waziri wa Ulinzi Angelina Teny, ni kinyume na mkataba wa amani wa 2018, uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Teny pia ni mke wa Machar.

Waziri wa masuala ya baraza la mawaziri Martin Elia Lomuro anasema kwamba mabadiliko yaliyofanywa na Kiir yalitekelezwa kwa nia njema kwa minajili ya kiutawala.

Tume ya Usimamizi na Uangalizi iliyoratibiwa upya, RJMEC, imetwikwa jukumu la kusimamia mkataba dhaifu wa amani wa Sudan Kusini. Meja jenerari Charles Gituai ambaye ni mwenyekiti mwandamizi wa tume hiyo anasema kwamba Kiir na Machar ni lazima watafute suluhu kwa mzozo uliopo.

XS
SM
MD
LG