Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 01:44

Mzee Mandela alazwa hospitali


Rais mstaafu Nelson Mandela
Rais mstaafu Nelson Mandela

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela ni shujaa wa kitaifa na kimataifa aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela amelazwa hospitali tena baada ya kuugua mapafu. Taarifa kutoka ofisi ya rais Jacob Zuma inasema bw. Mandela alilazwa hospitali Jumatano usiku baada ya kuugua tena mapafu, tatizo lililomfanya alazwe hospitali kwa wiki tatu mwezi Desemba mwaka jana.

Bw. Zuma Alhamis alimtakia mshindi huyo wa tuzo la amani la Nobeli nafuu ya haraka na kueleza imani yake juu ya timu ya madaktari wanaomhudumia mzee Mandela.

Bw. Mandela alitumika kifungo cha takriban miongo mitatu jela kwa kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na kuwa shujaa wa kitaifa akiongoza serikali ya kidemokrasia baada ya utawala wa manyanyaso na ubaguzi kutoka kwa wazungu waliokuwa wachache. Alichagukiwa kuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Serikali ya Afrika Kusini imeitaka jamii ya kimataifa kumwombea rais huyo mstaafu wakati anapougua.
XS
SM
MD
LG