Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 19:51

Mwili wa Mandela wawasili Qunu


Msafara uliosindikiza mwili wa marehemu Nelson Mandela hadi Qunu Dec.14, 2013
Mwili wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela umesafirishwa hadi Qunu, kijiji alichokulia kiongozi huyo wa zamani na mpiganaji dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Maelfu ya watu walisimama kwenye barabara na mitaa Jumamosi kumwaga shujaa huyo wa ukombozi, huku maiti yake ikisafirishwa chini ya ulinzi mkali kutoka uwanja wa ndege wa Mtatha hadi kijiji hicho cha Qunu. Wengi walikuwa na hisia mchanganyiko, za heshima kwa Mzee Mandela na majonzi kwamba ameondoka duniani.

Hema kubwa imeezekwa huko Qunu tayari kwa mazishi ya marehemu Mandela yatakayofanyika kesho Jumapili. Mazishi hayo yatahudhuriwa na familia ya Mandela na wageni wachache walioalikwa.

Mapema Jumamosi chama tawala cha African National Congress kilifanya ibada ya kumbukumbu kwa rais huyo wa zamani huko Waterkloof kabla ya maiti yake kusafirishwa katika mkoa wa Eastern Cape.

Mandla Mandela, mjukuu wa marehemu alisema babu yake aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 95 aliendelea kujitolea kuimarisha maisha ya watu hata baada ya kustaafu kutoka siasa.
XS
SM
MD
LG