Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 22:59

Mwezi wa Ramadhan ukiendelea Sudan yakabiliwa na njaa


Sudan wiki hii imeingia katika siku ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa katika vita ambavyo vimefanya sehemu nyingi za nchi kukabiliwa na njaa.

Baadhi ya wakazi nchini humo hasa katika mji mkuu wa Khartoum, wamesema hili si jambo la kushangaza kwa sababu wamekuwa katika hali hiyo kwa miezi kadhaa.

Wanasema wamekuwa wakila mlo mmoja kwa siku kwa miezi kadhaa, na hawana njia ya kujikwamua kutoka katika hali hiyo. Kwa kipindi hiki cha Ramadhan, wakazi hao wamekuwa wakitegemea futari zinazo andaliwa misikitini ambapo pia huwa na chakula kichache.

Vita hivyo vinavyo karibia miezi 11 sasa, ambavyo vinatokana na uhasama baina ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan wa jeshi la nchi dhidi ya Mohamed Hamdan Daglo, wa vikosi vya akiba vya RSF, umesha sababisha vifo vya maelfu ya watu, kuwakosesha makazi mamilioni, na kuharibu miundombinu ya nchi.

Forum

XS
SM
MD
LG