Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:07

Mwenyekiti wa chama cha NLD Tanzania afariki


Mwenyekiti wa chama cha NLD
Mwenyekiti wa chama cha NLD

Taarifa kutoka hospitali ya Nyangao imethibitisha kifo cha Dakta Emmanuel Makaidi ambaye pia alikuwa akigombea ubunge anayeiwakilisha UKAWA katika jimbo la Masasi mjini kupitia chama chake cha NLD.

Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, dakta Emmanuel Makaidi amefariki dunia Alhamisi katika hospitali ya Nyangao Mkoani Lindi.

Taarifa kutoka hospitali ya Nyangao imethibitisha kifo cha Dakta Emmanuel Makaidi ambaye pia alikuwa akigombea ubunge anayeiwakilisha UKAWA katika jimbo la Masasi mjini kupitia chama chake cha NLD.

Kifo cha Dakta Emmanuel Makaidi kinachodaiwa kutokana na shinikizo la damu, kitasababisha pia kuahirishwa kwa uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Masasi kama ilivyotokea kwa majimbo mengine manne yaliyopoteza wagombea kupitia vyama mbambali ambayo ni jimbo la Lushoto mgombea wa CHADEMA , Ulanga Mashariki mgombea wa CCM , jimbo la Arusha, Mgombea wa ACT na Jimbo la handeni mgombea wa CCM.

Chama cha NLD kimejiunga na UKAWA kuungana na vyama vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI na CUF ambapo wamesimamisha mgombea mmoja wa Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na kuachiana majimbo kadhaa ya udiwani na ubunge.

XS
SM
MD
LG