Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 04:12

Mwenyekiti wa AU akemea mfumo dume barani Afrika


Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Umoja wa Afrika umeanza kikao chake cha wiki nzima huko nchini Rwanda huku mataifa yote yakiombwa kutoa nafasi sawa kati ya wanawake na wanaume ikiwa bara hilo linahitaji kupiga hatua zaidi. Mwenyekiti wa kamati ya umoja wa Afrika Dr. Nkosazana Dlamin Zuma alizitaka ngazi husika kukomesha mfumo dume ambao yeye ameutaja kama ndio unaodumaza maendeleo ya bara hilo.

Suala la haki za wanawake na haki za binadamu zimeonekana kutawala katika kikao hiki ambapo Dr.Lamin Zuma alionekana kulalamikia tabia ya mfumo dume ambao bado unatawala barani Afrika.

Alisema kwa mfano tunapozungumzia asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake ambayo hata si sawa baadhi ya wanaume wanakuja juu kwa ukali na kusema kuwa wamegeuka viumbe walioko hatarini lakini kimsingi bado wanamiliki asilimia 70 ya nafasi za ajira huku wao wakiwa chini tu ya asilimia 50 ya wakazi wote wa mataifa yetu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Pia moja ya ajenda muhimu inayosubiriwa ni kujua nani atakayerithi kiti cha Dr. Nkosazana lamin Zuma. Ambaye ndie mwenyekiti wa sasa wa umoja wa Afrika anayemaliza muda wake.

XS
SM
MD
LG