Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:49

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu ICC anaitembelea Israel

 Karim Khan, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC).
Karim Khan, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC).

“Ziara hiyo ambayo sio ya kuchunguza mazingira yaliopo, inawakilisha fursa muhimu ya kuonyesha huruma kwa waathirika wote na kushiriki katika mazungumzo,” mahakama hiyo iliandika kwenye mtandao wa X, zamani ukijulikana Twitter.

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), Karim Khan aliitembelea Israel “kwa ombi na mwaliko” wa manusura na familia za waathirika wa mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7, ICC imesema Alhamisi.

“Ziara hiyo ambayo sio ya kuchunguza mazingira yaliopo, inawakilisha fursa muhimu ya kuonyesha huruma kwa waathirika wote na kushiriki katika mazungumzo,” mahakama hiyo iliandika kwenye mtandao wa X, zamani ukijulikana Twitter.

Khan pia anatarajiwa kusafiri hadi Ramallah katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi ambako atakutana na maafisa waandamizi wa Palestina, ICC imesema.

Wanamgambo wa Hamas waliwachukua mateka wapatao 240 kutoka kusini mwa Israel, wakati wa shambulio la Oktoba 7 ambalo maafisa wa Israel wanasema liliuwa watu 1,200 wengi wao wakiwa raia.

Forum

XS
SM
MD
LG