Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akithibitisha rasmi kwa mara ya kwanza kukamatwa kwa Durov tangu alipokuwa anashikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Le Bourget nje ya Paris siku ya Jumamosi jioni, alisema hakukamatwa kwa sababu za kisiasa, licha ya maoni mengi ya uongo mtandaoni.
“Kukamatwa kwa rais wa Telegram kwenye ardhi ya Ufaransa kulifanyika kama sehemu ya uchunguzi wa mahakama unaoendelea,” Macron aliandika kwenye mtandao wa X.
“Huu sio hata kidogo uamuzi wa kisiasa. Ni jukumu la majaji kuamua,” aliongeza.
Katika taarifa iliyofuata, mwendesha mashtaka wa Paris Laure Beccuau alisema Durov alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya mtu ambaye hakutajwa jina ulioanzishwa na kitengo cha uhalifu wa mtandaoni tarehe 8 Julai.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Durov anaweza kuendelea kushikiliwa hadi Jumatano.
Forum