Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:46

Waandishi Sudan Kusini wataka mwenzao aachiliwe huru


Oliver Modi, kushoto, mwenyekiti wa Umoja wa Wanahabari nchini Sudan Kusini
Oliver Modi, kushoto, mwenyekiti wa Umoja wa Wanahabari nchini Sudan Kusini

Mwandishi wa habari alizuiliwa wiki moja iliyopita baada ya kuwasiliana na msemaji wa kikundi cha waasi kwa kutafuta habari

Muungano wa Waandishi wa Habari nchini Sudan Kusini unatoa wito kwa serikali kumwachilia huru Jackson Ochaya, mwandishi wa habari ambaye alizuiliwa wiki moja iliyopita baada ya kuwasiliana na msemaji wa kikundi cha waasi kwa kutafuta habari.

Mwanafamilia aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa kuogopa kulipiziwa kisasi aliliambia gazeti la Ochaya kwamba maafisa wa Usalama wa Kitaifa (NSS) wanamshikilia mwandishi huyo kwenye makao yao makuu yao huko Jebel.

Ochaya huenda anazuiliwa kwa sababu aliwasiliana na msemaji wa waasi wa National Salvation Front (NAS) ili kutoa maoni juu ya makala aliyokuwa akiandika, kulingana na Oliver Modi, mwenyekiti wa Umoja wa Wanahabari nchini Sudan Kusini. Mnamo Agosti 31, NSS ilimwita Ochaya na kaimu mhariri mkuu wa gazeti hilo, Stella Kiden, makao makuu yao kuhojiwa.

“Usalama wa taifa ulihoji tu waandishi wa gazeti hilo liitwalo The Number 1 Citizen juu ya jinsi walivyoamua kuandika habari hiyo na haswa mawasiliano yao na NAS. Hiyo ndiyo sababu ya kila kitu, lakini kulingana na mwandishi wa habari, hii ni kutafuta mizania ya habari kwa mujibu wa kanuni za uandishi unapoandika hiyo haipaswi kuwa habari ya upande mmoja,” Modi aliiambia Sauti ya Amerika.

Kiden alisema NSS ilimwachilia yeye na Ochaya Jumatatu jioni, kisha ikamtaka Ochaya kurudi siku iliyofuata kuchukua kitambulisho chake.

Kiden alisema Ochaya alirudi kazini Septemba mosi lakini baadaye aliomba ruhusa ya kuondoka ili aweze kukutana na mjomba wake ambaye alikuwa amemtaka Ochaya akutane naye katika eneo la makazi la Thingpiny. Hiyo ilikuwa mara ya mwisho wao kumuona.

XS
SM
MD
LG