Muda mfupi baada ya kuachiliwa kwa mwanahari huyo Nazila Maroufian kutoka kwenye jela ya Evin mjini Tehran aliweka ujumbe kwenye mtandao wa X pamoja na Instagram ukiwa na picha yake akishikilia maua mkono mmoja huku akiunyoosha mkono mwingine na kuonyesha ishara ya ushindi.
Maroufian ambaye umri wake ulitajwa kuwa miaka 23 na chombo kimoja cha habari cha Uajemi, Oktoba mwaka uliopita, alifanya mahojiano kwenye jukwa la mtandao la Mostaghel na Amjad Amini ambaye ni baba yake Mahsa Amini ambaye alifia jela baada ya kukamatwa kwa madai ya kukiuka kanuni ya kuvaa hijab, na kupelekea maandamano makubwa Septemba mwaka jana kote nchini Iran.
Forum