Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:55

Mwanasiasa mkongwe wa Tanzania afariki dunia


Picha ya mchungaji Christopher Mtikila

RPC Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao wamejeruhiwa.

Vyombo vya habari nchini Tanzania vinaripoti kwamba Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Jumapili alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

RPC Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na alikuwa na watu wengine watatu katika gari hilo ambao wamejeruhiwa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.

Mchungaji mtikila atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa wanasiasa hasa wa upinzani waliokuwa saidia kuleta chahcu katika siasa ya vyama vingi.

Ujasiri wake katika upinzani ulikwenda mbali hapa mara nyingine alikuwa tayari kufungwa jela akitetea demokrasia na uhuru wa kuzungumza katika masuala ya siasa.

Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu.

XS
SM
MD
LG