Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:42

Wanaharakati waitaka Polisi kumwachilia wakili wa haki za binadamu Uganda


Wakili maarufu wa haki za binadamu Uganda Nicholas Opio akiwa amembeba mteja wake Stella Nyanzi Opio kutoka mahakamani mjini Kampala Uganda, May 10, 2017. (Photo: H. Athumani/VOA)
Wakili maarufu wa haki za binadamu Uganda Nicholas Opio akiwa amembeba mteja wake Stella Nyanzi Opio kutoka mahakamani mjini Kampala Uganda, May 10, 2017. (Photo: H. Athumani/VOA)

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Uganda wanatoa wito kwa serikali kumwachilia huru wakili wa haki za binadamu Nicholas Opio, ambaye alikamatwa Jumanne kwa madai ya biashara ya kutakatisha fedha. Wafuasi wanasema Opio anatuhumiwa kwa uanaharakati wake.

Kikundi cha mawakili na wanaharakati walikwenda kwenye Kitengo Maalum cha Upelelezi cha polisi wa Uganda Jumatano kudai kumwona Opio na kuwataka polisi wamwachilie huru.

Opio, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la haki za binadamu Chapter 4 nchini humo, alikamatwa Jumanne na wenzake wawili katika mgahawa mmoja jijini Kampala.

Kulingana na Chapter 4, Opio amekuwa akikusanya ushahidi kuhusiana na mauaji na ukamataji ambao ulitokea wakati wa siku mbili za maandamano nchini Uganda yaliyoanza Novemba 18.

Watu 56 waliuwawa katika mapigano kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji aliyeingia kwenye siasa Bobi Wine, kiongozi wa chama cha National Unity Platform. Wakili wa haki za binadamu Elone Kiiza anasema Opio yupo kwenye ari nzuri. Lakini haamini Opio ataachiliwa katika saa 48 za kawaida.

“Hawajamfungulia mashitaka rasmi. Na bado hawajachukua maelezo yake. Tunaendelea kufuatilia hali ikiwa watakubali kumwachilia kwa dhamana au kumfungulia mashitaka.” Elone alisema.

Msemaji wa polisi Fred Enanga anasema polisi na Mamlaka ya Ujasusi wa Fedha wa Uganda wamekuwa wakimfuatilia Opio na wana sababu za kumkamata.

XS
SM
MD
LG