Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:35

Mwanasheria wa Dr Besigye kufungua kesi


Mwanasheria wa kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, kutoka chama cha “Forum for Democratic Change (FDC) anapanga kufungua mashitaka dhidi ya serekali.

Kesi hiyo atafungulia mjini Kampala, baada ya kushutumu polisi na idara nyingine za usalama kwa kukiuka haki za mteja wake.

Polisi walimzuia Dr Besigye, asihudhurie mkutano uliopangwa awali na mwanasheria Ladislaus Rwakafuzi, Jumatano asubuhi katika mji mkuu wa Kampala.

Alichukuliwa kwa nguvu mpaka kituo cha polisi baada ya watu kukusanyika katika ofisi za mwanasheria wake.

Katika mahojiano na VOA, Rwakafuzi, amesema polisi wa nchini humo hawatendi haki na kumtendea isivyo sawa Besigye toka alipoamua kushindana na rais Yoweri Museveni katika uchaguzi.

XS
SM
MD
LG