Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:36

Mwanariadha wa Ethiopia asaidiwa


Mwanariadha wa mbio za marathoni wa Ethiopia, Feyisa Lelisa, aliyeshinda medali ya fedha katika Olympic ya Rio 2016 iliyomalizika, amezusha habari duniani kwa kuonyesha ishara ya kugomea yanayofanyika katika eneo la Oromia nchini Ethiopia.

Ishara hiyo ya kisiasa inamuweka mwanariadha huyu mashakani na sasa baadhi ya Wa-Ethiopia wanaoishi nje wanataka kumsaidia.

Solomon Ungashe anayeishi jimboni California ni mmoja wa watu watatu waliofungua akaunti ya mtandaoni ya kumsaidia mkimbiaji huyo.

Ungashe ameiambia VOA kwamba mwanariadha huyo hakuomba kufanyiwa hilo lakini mashabiki wake ndio walioamua baada ya kuona haja ya kufanya hivyo, na wamefanikiwa kukusanya dola za kimarekani 100,000 mpaka sasa.

Wameshatuma watu watatu kwenda jijini Rio de Jeneiro, Brazil, kumpatia msaada.

XS
SM
MD
LG