Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 19:19

Mwanamfalme wa Denmark kuchukua madaraka baada ya mama yake kujiuzulu

(FILES) (kutoka kushoto) Mwanamfalme wa Denmark Frederik, Malkia Margrethe II wa Denmark Prince Joachim wa Denmark wakiwasili katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya miaka 83, huko katika Kasri ya Amalienborg Copenhagen Aprili 16, 2023.

Mwanamfalme wa Denmark Frederik atakuwa mfalme baada ya mama yake, Malkia Margrethe II, mfalme aliyehudumu kwa  muda mrefu zaidi barani Ulaya, kutangaza Jumapili (Desemba 31) kuwa atajiuzulu Januari 14 baada ya miaka 52 ya kukalia kiti cha ufalme.

Malkia Margrethe II akitoa hotuba ya Mwaka Mpya akitangaza kuachia madaraka, Copenhagen, Denmark
Malkia Margrethe II akitoa hotuba ya Mwaka Mpya akitangaza kuachia madaraka, Copenhagen, Denmark

Malkia mwenye umri wa miaka 83, ambaye alipanda kiti cha enzi mnamo 1972, alitoa tangazo hilo la mshangao kwenye TV ya moja kwa moja wakati wa hotuba yake ya mkesha wa Mwaka Mpya, ambayo hutazamwa na watu wengi katika nchi yenye watu milioni 5.9.

Malkia huyo alishikilia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi barani Ulaya baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza mnamo Septemba 2022. Mnamo Julai, alikua Malkia aliyekaa muda mrefu zaidi katika historia ya Denmark.

Mwanamfalme Frederik atakuwa Mfalme Frederik X. Frederik alifunga ndoa na Mary Elizabeth Donaldson, raia wa Australia, mwaka wa 2004 na wanandoa hao wana watoto wanne.

Nchini Denmark, mamlaka rasmi yanakaa kwa bunge lililochaguliwa na serikali. Mfalme anatarajiwa kukaa mbali na siasa za upendeleo, akiwakilisha taifa kwa majukumu ya kitamaduni kutoka kwa ziara za serikali hadi sherehe za siku ya kitaifa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG