Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 14:59

Mwanamfalme Harry anahudhuria kutawazwa kwa Mfalme Charles III


Mwanamfalme Harry
Mwanamfalme Harry

Mke wa Harry, Meghan, Duchess wa Sussex atabaki California nchini Marekani akiwa na watoto wao wawili Mwanamfalme Archie na Binti mfalme Lilibet Kasri ya Buckingham imesema

Mwanamfalme Harry atahudhuria kutawazwa kwa baba yake Mfalme Charles III huko Westminster Abbey hapo Mei 6 Kasri ya Buckingham ilisema Jumatano na kumaliza miezi kadhaa ya uvumi kuhusu uwepo wake.

Mke wa Harry Meghan, Duchess wa Sussex, atabaki California nchini Marekani akiwa na watoto wao wawili, Mwanamfalme Archie na Binti mfalme Lilibet, ikulu hiyo imesema.

Tarehe ya kutawazwa ina-ambatana na siku ya kuzaliwa ya mtoto wao mkubwa Archie. Kuhudhuria kwa Harry kunakuja licha ya mpasuko ndani ya House of Windsor uliosababishwa na uamuzi wa Harry kufichua siri za familia katika kitabu chake kinachouzwa zaidi kinachoitwa Spare.

Ufichuzi huo ulijumuisha maelezo ya mazungumzo ya faragha na baba yake pamoja na kaka yake mkubwa Mwanamfalme William. Ufichuzi huo ulizua mivutano kati ya Harry na familia yake ambao ulikuwa hadharani wakati yeye na mkewe walipohamia marekani mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG