Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:34

Mwanajeshi wa UN auawa DRC


Mpango wa amani wa miaka miwili nchini DRC ulivunjika wakati kundi moja linaloongozwa na Ntaganda lilipojitenga na waasi waliungana tena na kujiita M23

Mlinzi wa amani mmoja wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC aliuawa na mlipuko wa kombora wakati kundi la waasi katika eneo la mashariki lenye mgogoro nchini humo likipambana kuteka mji wa Bunagana katika mpaka na Uganda.



Msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini Congo, Madnodje Mounoubai, alisema mlinda amani huyo raia wa India aliuwawa Alhamis usiku wakati wapiganaji kutoka kundi la uasi la M23 walipojaribu kuuteka mji wa Bunagana.

“Ninatangaza kifo cha mlinda amani mmoja raia wa India anayefanya kazi kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Congo. Alipigwa na mlipuko wa kombora wakati wa shambulizi lililofanywa na waasi wa M23 katika mji wa Bunagana Alhamis usiku”.

Mpango wa amani wa miaka miwili nchini DRC ulivunjika mwezi April wakati kundi moja la jeshi linaloongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda lilipojitenga. Walikimbilia msituni ambapo walijiunga tena kama waasi wa M23 ikiwa ni tarehe ya machi mwaka 2009 wakati waasi wa zamani walipotia saini mkataba na serikali ya Congo na kuwaruhusu kuungana na jeshi la serikali lililopo wakati huu na kuongeza nguvu zaidi.

Baada ya kudhibiti maeneo ya juu waasi wiki hii waliingia na kuteka kijiji cha Jambo kinachokatisha kuingia kwenye mji wa Bunagana uliopo mpakani mwa Uganda na Rwanda.Waasi waliuteka mji wa Bunagawa Alhamis usiku, kwa mujibu wa msemaji wa waasi pamoja na wakazi wa mji ambao waliomba wasitajwe majina wakikhofia usalama wao.


XS
SM
MD
LG