Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:31

Mwanaharakati wa mazingira Wangari Maathai aagwa rasmi


Mwanaharakati wa mazingira Wangari Maathai aagwa rasmi
Mwanaharakati wa mazingira Wangari Maathai aagwa rasmi

Mamia ya watu jumamosi wamefurika katika bustani ya Uhuru Park mjini Nairobi Kenya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Wangari Maathai

Mamia ya watu jumamosi wamefurika katika bustani ya Uhuru Park mjini Nairobi Kenya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Wangari Maathai aliyefariki dunia jumapili baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Saratani.

Bi. Maathai alikuwa mwanamke wa kwanza afrika kupata tuzo ya nobel ya amani, akiwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na wanyonge na pia utunzi wa mazingira.

Ameagwa leo katika maziko yaliyoshuhudiwa siyo tu wananchi wa Kenya bali pia na wawakilishi kutoka nje ya nchi. Mbali na rais Mwai Kibaki wa Kenya na waziri mkuu Raila Odinga , Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania aliwakilishwa na waziri wake Bi. Anna Tibaijuka. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon pia aliwakilishwa.

Katika hotuba za maziko Bi . Maathai amekumbukwa kwa kuanzisha kampeni za utunzi na utetezi wa mazingira tangu miaka 1970 ambapo tangu wakati huo karibu miti milioni 50 imepandwa Kenya kufuatia juhudi zake.

XS
SM
MD
LG