Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 13:35

Mwanaharakati mashuhuri nchini Misri asamehewa na Rais al-Sisi


Mwanaharakati wa Misri Ahmed Douma, akiwa katika chumba cha Mahakama ya New Cairo, nje kidogo ya Cairo. Picha ya Reuters
Mwanaharakati wa Misri Ahmed Douma, akiwa katika chumba cha Mahakama ya New Cairo, nje kidogo ya Cairo. Picha ya Reuters

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amewasamehe wafungwa kadhaa akiwemo mwanaharakati mashuhuri Ahmed Douma, televisheni ya serikali imesema Jumamosi.

Douma, ambaye aliongoza maandamano ya kutetea demokrasia yaliyomuondoa madarakani rais Hosni Mubarak mwaka 2011, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2019 kwa kufanya vurugu na kuwashambulia maafisa wa usalama.

Akitoa hukumu yake wakati huo, Jaji alisema Douma alikuwa miongoni mwa umati wa watu waliovamia bunge na kuharibu sehemu ya jengo hilo, akiwaelezea kuwa walifanya kazi ya “shetani.”

Kama wanaharakati wengine kadhaa nchini Misri, Douma alifungwa jela chini ya utawala wa Mubarak, uongozi wa baraza la kijeshi uliofuata, chini ya utawala wa rais wa zamani Mohamed Mursi, na rais al-Sisi.

Mwezi uliopita, mamlaka zilimuachia huru pia mtafiti wa haki za binadamu Patrick Zaki na wakili Mohamed el-Baqer baada ya kusamehewa na rais al-Sisi.

Forum

XS
SM
MD
LG