Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 21:57

Mwanahabari wa Iran aliyeachiliwa jela Jumapili akamatwa tena


Mwandishi wa habari wa Iran Nazila Maroufian kwenye picha ya awali baada ya kuachiliwa Jumapili.Aug. 13, 2023.
Mwandishi wa habari wa Iran Nazila Maroufian kwenye picha ya awali baada ya kuachiliwa Jumapili.Aug. 13, 2023.

Mamlaka za Iran Jumanne zimemkamata tena mwandishi wa habari aliye hoji baba wa mwanamke ambaye kifo chake akiwa kizuizini cha polisi  kilizua maandamano makali nchini humo.

Mwanadada huyo amekamatwa tena siku mbili tu baada ya kuachuliwa kutoka jela. Nazila Maroufian aliachiliwa kutoka jela ya Evin mjini Tehran Jumapili, wakati akiweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii bila kuvaa hijab, ambayo ni hatia kwenye taifa hilo la kiislamu.

Ujumbe wake pia ulikuwa na maneno ya, “ Usikubali utumwa, unastahili kuwa huru”. Baada ya kukamatwa tena Maroufian alipelekwa kwenye jela ya wanawake ya Qarchak, nje ya Tehran ambayo hali yake imekuwa ikilalamikiwa na makundi ya haki za binadamu, shirika la habari la wanaharakati wa haki hizo la HRANA lenye makao yake makuu Marekani limesema.

Shirika hilo ambalo hukusanya taarifa kutoka kwa wanaharakati kote ulimwenguni limesema kwamba limedhibitisha ukamataji huo kutoka kwa jamaa wa karibu na Maroufian.

Forum

XS
SM
MD
LG