Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:42

Mwanadiplomasia Saudia: Pande zinazopingana Sudan kurejea kwenye mazungumzo Jumapili


Wanajeshi wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum tarehe 23 Aprili 2023. Picha na Rapid Support Forces/ AFP.
Wanajeshi wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum tarehe 23 Aprili 2023. Picha na Rapid Support Forces/ AFP.

Jeshi la Sudan linalopigana na kikosi cha RSF watarejea kwenye meza ya mazungumzo siku ya Jumapili, mwanadiplomasia mwandamizi wa Saudia Arabia  alisema hayo huku mashambulizi ya anga na mapigano makali yakiendelea usiku kucha kuzunguka  Khartoum licha ya makubaliano ya kuwalinda raia.

Saudi Arabia, ambayo imekuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, pia ilimwalika mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan kwenye mkutano wa Ijumaa wa Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu huko Jeddah, mwanadiplomasia huyo aliongeza.

Mzozo huo uliozuka ghafla mwezi mmoja uliopita umesababisha vifo vya mamia ya watu, kupelekea zaidi ya watu 200,000 kukimbilia katika nchi jirani, kuwakosesha makazi wengine 700,000 ndani ya nchi na hatari kwa mataifa ya nje kujihusisha na hivyo kuliyumbisha eneo hilo.

Licha ya kualikwa kwa Burhan kwenye mkutano wa Jeddah, hatarajiwi kuondoka Sudan kwa sababu za kiusalama, wanadiplomasia wengine wawili katika Ghuba walisema.

Burhan alialikwa kwa sababu yeye ni mkuu wa Baraza Kuu la Sudan ambalo lilikusudiwa kusimamia mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia kabla ya mzozo kuzuka, mwanadiplomasia wa Saudi Arabia alisema. Mpinzani wake ambaye ni mkuu wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti, ndiye naibu mkuu wa baraza hilo.

XS
SM
MD
LG