Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 07:38

Gbagbo azingirwa Abidjan na wapiganaji wa Outtara


wanjeshi wanaomuunga mkono kiongozi Ouattara wakiwa katika mapambano

Mji mkuu wa biashara wa Ivory Coast umezingirwa na wapiganaji wanaomunga mkono kiongozi anaetambuliwa na Jumiya ya kimataifa Alassane Outtara.

Wapiganaji wa majimbo ya kaskazini wanaomuunga mkono Outtara walifika nje ya nji wa Abidjan Alhamisi baada ya kuteka miji kadhaa muhimu kutoka majeshi ya serikali ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Yamossukro.

Habari za kufika kwa wapiganaji haozimesababisha kuzuka kwa wasi wasi mkubwa katika mji huo wa biashara.Vyanzo vingi vya habari vinaeleza kwamba walinda amani wa Ufraansa wamepelekwa katika sehemu mbali mbali za mji huo ambako inaripotiwa kumetokea wizi mkubwa wa ngawira.

Mapema Alhamisi Afrika Kusini imesema mkuu wa utawala wa majeshi ya Ivory Coast, Jenerali Phillipe Mangou ameomba hifadhi nyumbani kwa balozi wake huko Abidjan pamoja na familia yake.

Bw Outtara alitoa taarifa Alhamisi jioni akieleza kwamba vikosi vinavyomunga mkono, vimewasili nje ya Abidjan, na ametoa wito kwa wapiganaji watiifu na Gbagbo kujisalimisha. Washauri wake wanatabiri kwamba itachukuwa muda wa masaa kadhaa kabla ya Bw Gbagbo kuondolewa madarakani.

XS
SM
MD
LG