Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 07:10

Mvutano wa madaraka ndani ya chama tawala Uganda-NRM


Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi
Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi
Utata umejitokeza katika uwongozi wa chama tawala cha muda mrefu cha Uganda NRM baada ya kutolewa taarifa inayotatanisha kwamba, Rais Yoweri Museveni amemteuwa Katibu Mkuu mpya wa chama chake.

Awali, baada ya mkutano wa tume ya wabunge na viongozi wa chama kukutana kwa siku mbili Ikulu, ilitangazwa kwamba Waziri asiye na wizara maalum Richard Todwong, atakua kaimu Katibu Mkuu wa chama na Waziri Mkuu Amama Mbabazi mwenye umri wa miaka 65, katibu mkuu wa hivi sasa ataendelea na majukumu yake kama mkuu wa serikali.

Lakini baadae gazeti la serikali New Vision, lilichapisha ripoti kueleza kwamba Todwong hajachaguliwa kamu katibu mkuu bali ilielezwa kwamba amepewa jukumu la kushughulikia kazi za kila siku na uhamasishaji wa NRM hadi mwakani.

Bw. Todwong ameviambia vyombo vya habari kwamba, "Tumekubaliana kimsingi kuwa Katibu Mkuu wa hivi sasa ana kazi nyingi kusimamia wizara 30 za serikali na idara zake hivyo itakuwa bora kusaidiwa kazi za chama."
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hata hivyo mbunge wa Samia-Bugwe wilaya ya Busia Mulimba John anasema viongozi wameweza kutanzua mzozo wao na wale wanaotuhumiwa kuhusika na kampebni hiyo watafikishwa mbele ya tume ya maadili ya chama. Anasema Bw. Mbambazi alikanusha tuhuma za kuongoza kampeni hiyo pamoja na mkewe Jacqueline, ambae ndiye mkuu wa Tawi la Wanawake katika NRM.

Vyanzo vya karibu na chama vinaeleza kwamba wakati wa mkutano huo wa Ikulu , Rais Museveni alicheza tepu yenye sauti inayozungumzia kampeni ya kumpinga kiongozi huyo wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
XS
SM
MD
LG