Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 07:04

Mvutano wa kamati ya usalama Marekani juu ya uchunguzi wa Russia


Devin Nunes

Wabunge muhimu wa Marekani wako kwenye mvutano juu ya kusitishwa uchunguzi waliokuwa wanaufanya kuhusiana na Russia kuvuruga kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Mvutano huo wa hivi karibuni unatokana na kufutwa ghafla kwa mahojiano yaliokuwa yamepangwa kufanyika wazi Ijumaa yanayo wahusisha maafisa wa usalama wa Marekani wa ngazi ya juu.

Devin Nunes, Mrepublikan anayewakilisha California ametoa hoja kuwa badala yake ilikuwa muhimu kulisikiliza suala hilo kwa siri kutoka kwa wakurugenzi wa idara ya makosa ya jinai (FBI) na usalama wa taifa (NSA).

Kamati inataka taarifa zaidi… ambayo inaweza kupatikana katika mkutano wa siri,” Nunes amewaambia waandishi katika mkutano uliofanyika kwa haraka.

Tangazo la kubadilika kwa mkutano huo ulizusha upinzani kutoka kwa wabunge wa Demokratik, ambao wameeleza kuwa Mkurugenzi wa FBI James Comey na Mkurugenzi wa NSA Admiral Mike Rogers walikuwa tayari wametoa ushuhuda siku ya Jumatatu.

Wakati wa mahojiano, Comey alithibitisha kwa mara ya kwanza kuwa maafisa wa usalama walikuwa wanachunguza uwezekano wa kuwepo mahusiano kati ya timu ya kampeni ya Rais Donald Trump na Russia.

XS
SM
MD
LG