Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:30

Mvua kubwa zauwa zaidi ya watu 25 Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museven
Rais wa Uganda Yoweri Museven

Nyumba 22 katika wilaya ya Bulambuli zilifunikwa na mchanga ulioporomoka. Vijiji vilivyoathiriwa ni pamoja na Sisiya, Buluganya, na Lusha.

Zaidi ya watu 25 wamefariki dunia kufuatia maporomoko ya udongo katika wilaya ya Bulambuli mashariki mwa Uganda. Maporomoko ya udongo yalitokea usiku wa kuamkia jumatatu kutokana na mvua kali.

Taarifa zinasema nyumba 22 katika wilaya ya Bulambuli zilifunikwa na mchanga ulioporomoka. Vijiji vilivyoathiriwa ni pamoja na Sisiya, Buluganya, na Lusha.

Wilaya ya Bulambuli iko karibu na mlima Elgon , huku watu wengi wakiishi juu ya mlima huo.

Kwa mujibu wa naibu waziri wa majanga Musa Ecweru watu 32 walifariki dunia huku wengine wakiwa bado wamefunikwa na matope. Zoezi la ufukuzi linaongozwa na askari jeshi wakishirikiana na wafanyakazi wa msalaba mwekundu.

Waziri Ecweru ameonya kuwa wakati mvua inazidi kuongezeka wanatarajia matukio mengi ya kuporomoka kwa udongo kuripotiwa kutoka maeneo yaliyo karibu na wilaya ya Bulambuli kama vile Manafwa, mbale, Sironko, Bududa na Kapchorwa. Wilaya hizo zipo mashariki mwa Uganda.

Hii si mara ya kwanza maporomoko ya udongo kutokea Uganda. Mwaka jana takriban watu 300 walifariki huko Bududa kwenye kijiji cha Nametsi.

XS
SM
MD
LG