Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:32

Muungano wa upinzani Tunisia kufanya maandamano licha ya kunyimwa kibali

Wanachama wa mashirika ya kutetea haki za binadamu wakiwa wamebeba mabango wakati wa maandamano, baada ya Rais wa Tunisia Kais Saied kuamuru vikosi vya usalama kukomesha uhamiaji haramu na kuwafukuza wahamiaji wote wasio na vibali, huko Tunis, Tunisia Februari 25, 2023. REUTERS

Muungano wa upinzani wa National Salvation Front nchini Tunisia ulisema siku ya Alhamisi kwamba utafanya maandamano siku ya Jumapili licha ya kunyimwa kibali na mamlaka nchini humo, huku kukiwa na msako mkali dhidi ya wakosoaji wakuu wa rais wa nchi hiyo.

Upinzani wa Tunisia unatazama jinsi mamlaka itakavyoshughulikia maandamano hayo na mengine yaliyoitishwa Jumamosi na chama chenye nguvu cha wafanyakazi, UGTT, kutokana na kukamatwa mfululizo kwa wakosoaji mashuhuri wa Rais Kais Saied.

Gavana wa Tunis alisema katika taarifa yake kuwa anakataa kutoa kibali cha maandamano ya Jumapili kwa sababu viongozi wa kundi hilo wanatuhumiwa kula njama dhidi ya usalama wa taifa.

Viongozi wa muungano wa National Salvation Front ni miongoni mwa wapinzani kadhaa wa rais waliokamatwa mwezi mmoja uliopita kwa madai ambayo upinzani unasema yanachochewa kisiasa.

XS
SM
MD
LG