Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:24

Muswada wa sheria wa kulinda haki ya wanawake kutoa mimba wakwama kwenye baraza la Seneti la Marekani


wanaharakati wanaotetea haki ya kutoa mimba waandamana nje ya Mahakama kuu ya Marekani, May 11, 2022. Picha ya AP
wanaharakati wanaotetea haki ya kutoa mimba waandamana nje ya Mahakama kuu ya Marekani, May 11, 2022. Picha ya AP

Wademocrats katika baraza la Seneti Jumatano wameshindwa kupitisha muswada wa sheria unaolinda haki ya wanawake kutoa mimba nchini kote kabla ya uamuzi unaosubiriwa wa mahakama ya juu ya Marekani, ambao unaweza kubatilisha au kuweka mipaka kwenye haki ya kikatiba inayowaruhusu wanawake kutoa mimba.

Katika baraza la Seneti ambalo limegawanyika kulingana na misimamo ya kisiasa, lenye Wademocrats 50 na Warepublican 50, karibu Wademocrats wote waliunga mkono muswada huo unaolinda haki ya wanawake kuondoa mimba, huku Warepublican wote wakiupinga. Muswada huo haukupitishwa kwa kura 51 dhidi ya 49.

Wademocrats wameshindwa kupata kura za kutosha ili kuondoa utaratibu wa kura 60 zinazohitajika ili muswada wa sheria upitishwe.

Muswada huo ulifikishwa Jumatano kwenye kikao cha baraza la Seneti na kiongozi wa walio wengi Mdemocrat Chuck Schumer baada ya maoni ya jaji mmoja wa mahakama ya juu yaliyovuja wiki iliyopita, ambayo yalionyesha kuwa majaji watano wenye msimamo wa kihafidhina kati ya tisa , wanaunga mkono kubatilishwa kwa haki ya kikatiba ya karibu miongo mitano inayowaruhusu wanawake kuondoa mimba.

XS
SM
MD
LG