Siku ya Alhamisi, kulikuwa na uvumi kwamba rais huyo mwenye umri wa miaka 70 anakaribia kujiuzulu. Lakini kufikia Ijumaa asubuhi, hali ilionekana kubadilika huku washirika wake wakimuomba kuendelea kupambana.
Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilikuwa kinatarajiwa kufanya kikao cha dharura cha bodi yake ya kufanya maamuzi saa nne asubuhi majira ya huko, kujadili mzozo huo ambao ulizidisha migawanyiko ndani ya chama.
Ramaphosa amekuwa akikabiliwa na shutma kali tangu mwezi Juni, wakati mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi alipowasilisha malalamiko kwa polisi, akidai kuwa Ramaphosa alificha wizi wa pesa taslimu katika shamba lake la Phala Phala, kaskazini mashariki mwa nchi.
Ramaphosa alikanusha kufanya makosa yoyote.
Facebook Forum